Loading...

NYANI WAZUA GOMZO KISUMU KWA KUWAONYESHA WANAWAKE ISHARA CHAFU

Loading...
Kenya. Nyani wenye kiburi kingi wamewafanya wakazi wa Korando, Kaunti ya Kisumu kuishi kwa hofu baada ya kuibuka na mbinu za kuwafanya kuwa waoga na kuona haya kila mara.

Kulingana na mkulima mmoja ambaye ni mmoja wa waliochoshwa na tabia ya nyani hao, wanyama hao hutumia milio na lugha za ishara za kuwafedhehesha wanawake ambao wengi huwa hawana nguvu za kupambana nao.

Kwa sababu hiyo, maisha ya wanawake yamefanywa kuwa magumu sana eneo hilo huku wanyama hao wakipiga kambi katika mashamba ya watu kuharibu mazao. 

"Fikiria nyani anaweka mikono yake kichwani kukuambia kuwa, mwanamke sio kitu cha kuogopa," Magdalene Jumbo, mkazi wa eneo hilo aliiambia Citizen TV.

Ili kujiokoa kutokana na vitisho vya nyani hao, wanawake wengi wameamua kuvaa suruali, kofia na kubeba mawe mikononi ili kujiweka tayari kwa lolote litakalo tokea. 

Pia watoto ni miongoni mwa watu katika hatari ya kuvamiwa na nyani hao kwa kuwa wengine huwafukuza na kuwanyang'anya chakula.

"Juzi alikuja na kumnyang'anya mjukuu wangu mkate," Magdalene alilalamika. 

Wanaume nao hulazimika sasa kupiga kambi katika mashamba ili kulinda mimea yao isiharibiwe na wanyama hao. 

"Hawalali hawa nyani. Huingia nyakati za usiku na kuvunja uzio. Hula mazao yetu na kuiharibu usiku," Odongo Bodo alisema. 

Sasa wakazi wanaitaka serikali kuingilia kati na kutafuta mbinu za kuwatoa wanyama hao katika maeneo wanakoishi watu na kuwarejesha porini ili kurejesha amani Korando.
Na Yohana Samwel.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
NYANI WAZUA GOMZO KISUMU KWA KUWAONYESHA WANAWAKE ISHARA CHAFU NYANI WAZUA GOMZO KISUMU KWA KUWAONYESHA WANAWAKE ISHARA CHAFU Reviewed by By News Reporter on 7/10/2019 09:37:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.