Loading...
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya soka ya Liverpool Daniel Sturridge ametoa ofa ya hadi pauni 30,000 (sawa na milioni 80 pesa ya Tanzania) kwa yeyote atakayesaidia kumregesha mbwa wake.
Mbwa wa Sturridge aliibwa akiwa kwenye nyumba yake nchini Marekani baada ya nyumba yake kuvunjwa jijini Los Angeles Marekani.
Sturridge,29, ambaye aliondoka Liverpool mwezi uliopita baada ya mkataba wake kukamilika amesema mbwa wake aliibiwa akiwa matembezini.
Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la BBC, Jumatano, Julai 10 mchezaji huyo rusha kipande cha video katika Instagram akionesha jinsi nyumba yake iliyopo West Hollywood ivyoharibiwa.
“Tutalipa kiasi chochote kile ili kumpata mbwa wetu,” amesema Sturridge.
“Yoyote atakayemrudisha mbwa wangu nitampa pauni elfu 30, kiasi chochote kile.” alisema.
Sturridge pia ametuma picha nne za mbwa huyo na pia video zinazoonyesha wanaume watatu waliojifunika nyuso wakiingia kwenye nyumba hiyo Jumapili, Julai 7.
“Yeyote anayewajua waliovunja nyumba yangu, nitakulipa utakacho. Ninamaanisha nisemacho. Nitatoa pesa yeyote ile – haijalishi thamani.” aliongeza kusema.
Sturridge, kwa saasa anahusishwa na uhamisho kuelekea klabu ya Aston Villa ambayo inarejea EPL msimu ujao utaoanza rasmi Agosti.

Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MSHAMBULIAJI WA ZAMANI WA LIVERPOOL ATANGAZA DONGE NONO KWA ATAKAYEMUONA MBWA WAKE
Reviewed by By News Reporter
on
7/11/2019 06:08:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: