Loading...
Huko Tunisia rubani wa shirika la ndege la Iraq awachangisha abiria mchango wa mafuta ili ndege iweze kuruka.
Tukio hilo la kushangaza limetokea katika uwanja wa ndege wa Kartaca. Mara baada ya ndege hiyo ya abiria ya shirika la ndege la Iraq kujaza mafuta uwanjani.
Pesa ya kulipia mafuta hayo haikuwepo. Mamlaka ya uwanja huo ikazuia ndege hiyo kuruka, Hapo ndipo rubani wa ndege hiyo alipoamua kutumia njia ambayo si ya kawaida kwa kuwachangisha abiria dola elfu 3 ili kuweza kulipia mafuta hayo.
Abiria waligoma kuchangia ndipo Ubalozi wa Irak nchini Tunisia ulipoingilia kati na kulipia gharama hiyo. Baada ya kulipa pesa hiyo ndege hiyo iliondoka ikiwa imechelewa.

Na Neema Joshua.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RUBANI ALIVYOWACHANGISHA ABIRIA MCHANGO WA MAFUTA
Reviewed by By News Reporter
on
7/30/2019 07:04:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: