Loading...

SIRI YA KUISHI MAISHA MAREFU DUNIANI

Loading...
Kundi moja la wataalamu wa moyo limeelezea masuala muhimu ambayo yanamsaidia mtu kuishi maisha marefu kama ifuatayo:-

1. Jiweke mbali na sigara
2. Epuka unene
3. Fanya mazoezi
4. Kula lishe bora
5. Hakikisha unacheki na kupima kiwango cha kolestero mwilini, shinikizo la damu na sukari na kuhakikisha viko katika kiwango kinachotakiwa. 

Uchunguzi huo umeonyesha kwamba watu wengi umri wa kuanzia miaka 50 ambao wanaishi kwa kufuata masharti hayo huwa na uwezo wa kuishi miaka 40 zaidi bila kupata shinikizo la damu na ugonjwa wa moyo, ambayo ni magonjwa makuu mawili yanayoua watu zaidi duniani. 

Wataalamu wamesema kwamba, kila mtu anayetaka kuishi maisha marefu anatakiwa kufuata ushauri ufuatao:

- Jiepushe kuvuta sigara au acha kuvuta sigara kabisa.
- Hakikisha BMI yako haizidi 25.
- Kila wiki pata dakika zisizopungua 150 za kufanya mazoezi ya kawaida. 
- Jitahidi kufuata maelekezo ya kula lishe bora ambayo ni: vikombe 4 na nusu vya matunda na mboga mboga kwa siku, samaki mara mbili au tatu kwa wiki. Usinywe sana vinywaji vyenye sukari, na kula chumvi isizidi miligram 1,500 kwa siku.
- Kiwango cha kolestero au mafuta katika damu yako kisizidi 200.
- Shinikizo lako la damu lisiwe zaidi ya 120 chini ya 80.
- Sukari katika damu iwe chini ya 100.

Na Geofrey Okechi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SIRI YA KUISHI MAISHA MAREFU DUNIANI SIRI YA KUISHI MAISHA MAREFU DUNIANI Reviewed by By News Reporter on 7/15/2019 04:37:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.