Loading...
Mwanamuziki maarufu kutoka Uganda, Bobi Wine, na mtesi wake wa muda mrefu Jose Chameleon wamechukua hatua ya kushangaza ya kutangamana ili kuliokoa taifa lao.
Jose Chameleon aliamua kufuata nyayo za Bobi Wine hivi majuzi baada ya kutangaza nia yake ya kutaka kujiunga na siasa.
Mnamo mwezi Juni, Chameleone alikiri kuwa alipata msukumo wa kujiunga na siasa kutoka kwa Bobi Wine, lakini lengo lake ni tofauiti na mwenzake kwani anapambania kuwania katika nafasi tofauti.
Huku Bobi Wine akiwa mshindi wa kiti cha ubunge mwaka wa 2017, kama mgombea huru, Chameleone kwa upande wake ana lenga kuwa meya wa jiji kuu la Kamapala.
Wasanii hao wawili walikutana mnamo Jumapili, Julai 14 baada ya miaka na wakapanga mikakati na kukubaliana kufanya kazi pamoja kwa ajili ya maslahi ya taifa la Uganda.
“Jose aliibua wasiwasi kuwa bado watu wengi wanamshuku hadi sasa.Tulikubaliana kuwa watu wote wanao mshuku wana sababu kutosha hususan baada ya kuweka historia ya kuimba pia kuunga mkono utawala wa Rais Museveni," alielezea Bobi Wine kwenye mtandao wake wa Facebook
Kupitia mkutano huo, viongozi hao wawili ambao bado ni vijana waliafikiana kuungana pamoja ili kuleta mabadiliko nchini Uganda.
Bobi Wine, ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi Ssentamu, amekuwa na wakati mgumu kama mbunge kwa sababu ya kukashifu vikali utawala wa Museveni.
Mbunge huyo aliteswa sana kwa kukamatwa mara kadhaa na bado anaendelea kusimama imara kuhusu mtazamo wake wa kisiasa kwa kudai siasa za zamani zinapaswa kufutiliwa mbali.
Bobi Wine anatazamiwa kugombea kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2021.

Na Geofrey Okechi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UGANDA: BOBI WINE AKUTANA NA 'ADUI' WAKE JOSE CHAMELEONE KWA MARA YA KWANZA
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
7/17/2019 05:24:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: