Loading...

MWANAMKE ADAI ALISHIRIKI NGONO NA SHEMEJIYE AKIJUA MUMEWE

Loading...
Mfanyabiashara aliyetambulika kama Kuditat Ajayi kutoka Afrika Kusini, ameimbia mahakama kwamba alishiriki ngono na shemejiye akidhani alikuwa mumewe. 

Mumewe Ajayi alikuwa amewasilisha kesi mahakamani akiomba kutalakakiana na mkewe.

Hata hivyo, mwanamke huyo alidai kwamba shemejiye aliwasili nyumbani kwao usiku wa manane na alimtambua tu baada ya kushiriki mapenzi naye kulingana na Briefly. 

"Nilikuwa katika chumba chetu cha kulala wakati shemeji yangu alifika nyumbani usiku na kuingia chumbani humo. Nilidhani alikuwa mume wangu kwani yeye ana mazoea ya kuja nyumbani saa za usiku na tunashiriki mapenzi kisha tunalala. Nilibaini alikuwa ni shemeji yangu pindi tu baada yake kufanya mapenzi na naye. Nilipomuuliza alidai kwamba alilala na mimi sababu mme wangu alikuwa amesafiri," mwanamke huyo alisema. 

Aliongeza kwamba alimshtaki jamaa huyo kwa wifi yake ambaye alimshauri asimwambie yeyote kuhusu kisa hicho kwa ajili ya kuwepo kwa amani katika familia.

Mwanamke huyo alikana mashtaka hayo na kuiomba mahakama kuitupilia mbali kesi hiyo kwa kuwa alikuwa angali anampenda mumewe. 

Hata hivyo jamaa anashikilia kutulia katika ndoa yao hiyo huku akimshutumu mkewe kwa kuwa mzinifu na kudai kwamba alipata mtoto mmoja nje ya ndoa.

"Wakati nilipomuoa, nilimkodishia nyumba kwa kuwa nina wake wengine ambao sikutaka waishi pamoja. Nilianza kupata fununu kutoka kwa majirani kwamba mke wangu alikuwa na uhusiano na mwanamme mwingine ila nilipuuza hadi pale ambapo mpenzi wake huyo alianza kudai kwamba mmoja wa watoto wetu ni wake. 

"Hatimaye mwanamme huyo aliamua kuja nyumbani lakini nilikataa kumfungulia mlango. Wakati nilipomuuliza mke wangu, alikiri kufanya mapenzi na jamaa huyo ila hakupata mimba," Akande aliiambia mahakama. 

Hakimu wa mahakama hiyo, Adeniyi Koledoye, aliwataka wawili hao kutulia na kusitisha uhasama baina yao hadi pale ambapo kesi hiyo itakapoamuliwa Alhamisi, Agosti 22.
Na Richard Owino.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MWANAMKE ADAI ALISHIRIKI NGONO NA SHEMEJIYE AKIJUA MUMEWE MWANAMKE ADAI ALISHIRIKI NGONO NA SHEMEJIYE AKIJUA MUMEWE Reviewed by GEOFREY MASHEL on 7/17/2019 05:18:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.