Loading...

WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA JARIDA JIPYA LA MASWALA YA AFYA

Loading...
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, imezindua jarida la afya ya jamii, ambalo litatumika kutoa taarifa mbalimbali zilizochambuliwa kisayansi na kuziweka katika lugha nyepesi ambayo itaeleweka na kila mtu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jarida hilo,  Waziri wa afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema jarida hilo litakuwa na umuhimu mkubwa sana hasa katika kuleta taarifa  kwa jamii zinazotoka katika wizara hiyo.

Amewaelekeza wataalamu, wahariri wa vyombo vya habari na wakurugenzi kutoa taarifa za afya katika jarida hilo ili taarifa zao  ziweze kuwafikia wananchi kwa urahisi kupitia jarida hilo zitakazo  wasaidia  wananchi.

“Kuanzishwa kwa jarida hili  kutasaidia sana kwa wananchi kupata taarifa sahihi zilizotoka  katika wizara hiyo na kuzijua kwa undani, pia ni wakati sasa kwa wataalamu,  wakurugenzi na wahariri wa vyombo vya habari kutoa taarifa kupitia jarida hili” amesema Ummy.

Pia amewaagiza wataalamu wa jarida  hilo kuhakikisha jarida hilo linapatikana kielecronic ili kila mtu aweze kulipata jarida hilo.

“Ni toe wito kwa wasimamizi wa jarida hili mhakikishe jarida hili linapatikana kielectrinic mimi pia sio muumini wa kusoma majarida ila  kama likipatikana kielectronic na mimi nitaweza kupata taarifa hizo” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo cha ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa yakuambukizwa na yasiyoya kuambukizwa Dkt Janneth Mghamba , jarida hilo ambalo linatumia takwimu mbalimbali hapa nchini ambazo zinachambuliwa kisayansi na kuziweka  katika lugha nyepesi.

“Jarida hili litatumika kutoa taarifa ambazo zimethibitishwa na ambazo  zimechambuliwa kisayansi ambazo zitakuwa zimewekwa katika mfumo rahisi na mwepesi” amesema Mghamba

Amesema jarida hilo litasaidia kujua nini wizara inafanya na namna wao wanavyoweza kushiriki katika kudhibiti magonjwa hayo na namna ya kuepukana magonjwa hatarishi.

Amesema jarida hilo ni la kwanza na litakuwa kama kioo cha wizara  ya afya, kioo cha sera kioo cha kutoa mwelekeo,ufasaha wa sayansi mbalimbali  ambazo zinafanyika ndani na nje ya nchi.

Nae Mhariri msaidizi wa jarida hilo Dkt Julius Massaga, amesema jarida hilo limetengenezwa kwa takribani mwaka mmoja kabla ya kuzinduliwa hivi leo litasaidia kutoa taarifa sahihi kwa jamii ambazo zimethibitishwa na wizara ya afya.

Jarida hilo ambalo limefadhiliwa na CDC Foundation kutoka Marekani na litakuwa linatoka mara nne kwa mwaka, lengo ni kutoa taarifa sahihi zinazoandaliwa na wizara ya afya kuwafikia wananchi kwa urahisi.

Amewataka wadau kuchangamkia fulsa hiyo kwa ajiri ya kutoa taarifa zao ili ziweze kuwafikia wananchi kiurahisi na kuzijua taarifa hizo ambazo zitakuwa zimethibitishwa na wizara na zitakuwa za uhakika.

“Ni wakati wa  wadau sasa kujitokeza kuchangamkia fulsa hii kwa kuleta taarifa ili taarifa zao ziwafikie wadau wao kwa sababu zitakuwa zinatoka katika sehemu sahihi” amesema Massaga
Na Geofrey Okechi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA JARIDA JIPYA LA MASWALA YA AFYA WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA JARIDA JIPYA LA MASWALA YA AFYA Reviewed by By News Reporter on 7/02/2019 06:13:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.