Loading...
Je wajua kuhusu Saratani ya mfuko wa mayai ya uzazi? Dundiika News itakusaidia kulijibu kwa usahisi swali hili.
Kabla ya kwenda mbali katika ufafanuzi zaidi kuhusu saratani hii, kwanza kabisa tufahamu kuhusu vifuko hivyo.
Mwanamke wa kawaida ana vifuko viwili vidogo vilivyo kila upande wa mfuko wake wa uzazi na vifuko hivyo ndivyo chimbuko la aina hii ya kansa. Lakini kwa mujibu wa tafiti, ni vigumu kuitambua.
Anayepata dalili za saratani hii ambazo huonekana ugonjwa ukiwa umeenea mno, ni muhimu kutembelea daktari kila mwaka kwa uchukuzi wa kina.
Saratani hii haibagui ila kuna walio kwenye hatari zaidi ya kuipata na ni wafuatao:
a. Ikiwa umewahi kuwa na saratani ya matiti
b. Wanawake wenye zaidi ya umri wa miaka 50 wako katika hatarini ya kuapata ugonjwa huu. c. Mwanamke tasa
d. Msichana anayepata hedhi katika umri mdogo
e. Ikiwa kuna mtu wa familia ambaye amewahi kuugua ugonjwa huu
Ikiwa itagunduliwa mapema, kama saratani yingine, mtu anaweza kupona kupitia matibabu na lise bora.
Vyakula vinavyofaa ili kuzuia ama kupunguza hatari na uwezekano wa mtu kupata saratani ya Mfuko wa Mayai ni ulaji mboga na matunda.
Ingawa ni vigumu kupata takwimu kamili za akina mama wanaougua ugonjwa huu au maafa yanayosababishwa nao Wanawake wengi hasa wanaoishi mashambani hufariki dunia pasi na kujua wanaugua saratani ya mfuko wa mayai ya uzazi.
Hata hivyo kuna changamoto kubwa ambayo huchangia pia katika idadi kuwa ya wanaoangamia kufuatia kansa hii kwani, gharama ya kupata matibabu ni ya juu mno na ni wachache wenye uwezo wa kugharamia matibabu.
Pia kuna haja ya kuelimisha kina mama umuhimu wa kutafuta matibatu au kuchunguzwa katika sehemu za uzazi mara kwa mara, ili kuepukana na gharama nyingi katika muda wa mbeleni wakati ugonjwa huo utakapokuwa umeenea zaidi ikiwa utagunduliwa.
Vilevile serikali kupitia kwa Wizara ya Afya ina jukumu la kuhakikisha inaweka kampeini za kudumu katika kuukabili au kuangamiza ugonjwa wa saratani nchini.

Na Yohana Ambilikile.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
FAHAMU KUHUSU KANSA YA KIZAZI, DALILI NA JINSI YA KUJIKINGA
Reviewed by By News Reporter
on
8/02/2019 11:21:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: