Loading...
Korea kaskazini imefyatua kombora la masafa mafupi ambalo halijabainika mara mbili , kwa mujibu wa maafisa wa Korea Kusini , katika jaribio la tatu la silaha hizo katika kipindi cha wiki moja pekee.
Ufyatuaji wa makombora hayo ulifanyika katika eneo la mwambao wa mashariki mwa taifa hilo mapema Ijumaa.
hatua hiyo inaonekana kama hatua ya taifa hilo inayolenga kujibu mazoezi ya kijeshi ya baina ya Korea Kusini na Marekani yanayotarajiwa kuanza mwezi huu.
Wakati huo huo Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimeitaka Korea kaskazini kushiriki maungumzo ya "maana " na Marekani.
baada ya mkutano wa faragha katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa , mataifa yalisema kuwa vikwazo vya kimataifa vinapaswa kuimarishwa hadi utawala wa Pyongyang utakapoangamiza mipango yake ya nyuklia makombora ya masafa.
Ufyatuaji wa makombora hayo ulifanyika katika eneo la Yonghung katika jimbo la South Hamgyong katika bahari ya Japan, inayofahamika pia kama Bahari ya Masharik , kwamujibu wa Mkuu wa kikosi cha pamoja cha Korea kaskazini na Korea Kusini (JCS).
Eneo hilo linaonekana kama kituo cha kufyatulia makombora ambacho hakijawahi kutumiwa awali , amesema Ankit Panda, afisa katika shirikisho la wanasayansi wa Marekani - Federation of American Scientists.
"Hiki ni kielelezo kingine cha enzi ya Kim Jong-un zaidi ya ufyatuaji wa makombora ya usiku : kufyatua kutoka vituo ambavyo havikuwahi kutumiwa awali au ambavyo havitumiwi ."
Akizungumza katika ikulu ya White House, rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa hana hofu na ufyatuaji wa hivi karibuni wamakombora kwasababu ni ya masafa mafupi na "ni ya kiwango cha kawaida ".
Jumatano , Korea Kaskazini ilirusha makombora mawili ya masafa yanayopaa kilomita 250 (maili 155 ) na kufikia urefu wa kilomita 30 kabla ya kutua kwenye bahari ya Japan, inayofahamika a Bahari ya mashariki , k wamujibu wa Korea Kusini.
Korea Kusini iliyatambua makombora hayo ya masafa kuwa yalikuwa ni aina tofauti na yaliyofyatuliwa awali . Lakini Alhamisi , Pyongyang ilitoa kauli tofauti , ikisema kuwa ilifanya majaribio ya mfump mpya wa ufyatuzi wa roketi, lakini haikutoa maelezo.
Mnamo Julai 25, Korea kaskazini ilifyatua makombora mengine mawili, moja likiwa na uwezo wa kusafiri takriban kilomita 690.
Ufyatuaji huo wa makombora ulikuwa ni wa kwanza kufanyika tangu Bwana Trump na kiongozi wa korea Kim Jong-un wafanye mkutano ambao haukupangwa mwezi Juni katika eneo lisilokuwa na silaha ,, ambalo linatenganisha Korea mbili , ambako walikubaliana kuanzisha mazungumzo ya kuacha matumizi ya nyuklia.

Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KOREA KASKAZINI "YACHAFUA" ANGA KWA MAKOMBORA
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
8/02/2019 09:22:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: