Loading...

FAIDA NA MAMBO MUHIMU 5 YA KUZINGATIA UNAPOTUMIA KONDOMU YA KIUME

Loading...
Katika ulimwengu wa leo, kuna njia nyingi za kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU). Njia mojawapo ni kwa wapenzi kufuata maadili ya dini na kuacha kushiriki tendo la ndoa nje ya ndoa.

Kama umeshindwa, basi unashauriwa kupunguza idadi ya washirika wa mapenzi na kuzingatia njia za kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya zinaa ikiwemo Ukimwi. Njia moja inayoshauriwa ni matumizi ya mipira ya kiume (Condom), matumizi sahihi ya mipira hii huweza kukukinga na maambukizi ya magonjwa ya zinaa ikiwemo virusi vya ukimwi na magonnjwa mengine. Pia, husaidia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa mengine yanayosambazwa kupitia tendo la kujamiina kama Zika au Ebola, bila kusahau mimba zisizo tarajiwa, hivyo matumizi ya kondomu yana faida kubwa sana kwa mwanamume.

Leo hii tutaangalia vitu vya msingi vya kuzingatia unapotumia mipira hii;

1. Hakikisha unatumia condom kila wakati unapofanya ngono, usiwe na machaguo ya kwa nani utatumia na kwa nani hautumiaa au kumuamini mtu kwa fikira. Jenga kuwa matumizi ya kondomu ni moja ya sehemu muhimu ya tendo lako la ndoa.

2. Hakikisha unatumia condom kabla ya kuanza ngono. Kuna baadhi ya watu huanza kwanza ngono bila kutumia condom na huvaa baadae wakiwa wanakaribia kumaliza. Kwa kufanya hivi, kunakuweka katika hatari ya kupata maambukizi ya ya magonjwa ya zinaa ikiwemo virusi vya VVU kwa sababu, viusi vya magonjwa haya havina mua maarumu, maambukizi hutokea pale tuu kunapokuwa na mazingira yanayowezesha muingiliano wao, kama machubuko ambayo si rahisi kuiona kwa macho.

3. Hakikisha condom unayotumia haijapita muda wake. Kwa kutumia kondomu iliyopita muda wake kunaweza kusababisha kupasuka ukiwa kwenye tendo na kukuweka katika hali ya hatari kupata maambukizi kwa sababu ni wachache sana hubaini kama kondomu imepasuka au kuwa na nguvu ya kuacha na kubadili kondomu pindi wanapoanza na kutokea upasukaji.

4. Hakikisha condom ipo kwenye hali yake ya uimara. Matumizi ya condom iliyoanza kupasuka au yenye vitobo huweza kupelekea kupasuka inapowamba na kukuweka kwenye hatari zaii.

5. Hifadhi kwenye hali inayotakiwa; Kuhifadhi conom kwenye mazingira yenye joto zaidi huathiri ubora wake

Unaweza kununua kondomu kutoka katika duka la dawa lolote lililo karibu yako.
Na Juma Ally.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
FAIDA NA MAMBO MUHIMU 5 YA KUZINGATIA UNAPOTUMIA KONDOMU YA KIUME FAIDA NA MAMBO MUHIMU 5 YA KUZINGATIA UNAPOTUMIA KONDOMU YA KIUME Reviewed by GEOFREY MASHEL on 8/10/2019 05:19:00 AM Rating: 5

Maoni 1 :

  1. Hyooooo ni kweli kabisaaa na unashauriwa kutumia 2kila iitwapo Leo

    JibuFuta

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.