Loading...
Ramesh Babu, mzaliwa wa India, alianza maisha yake kama mtoto wa kinyozi maskini ambaye aliaga dunia Ramesh akiwa mtoto.
Bilionea huyo alizifuata nyayo za babake na kuendeleza taaluma hiyo akiwa na umri wa miaka 14.
Mwaka 1994, mfanyabiashara huyo alifungua biashara yake kwenye gari la Maruti ambalo pia lilikuwa likihudumia kama duka la kinyozi baada ya kuhifadhi pesa kwa miaka kadhaa.
Kwa sasa mfanyabiashara huyo ni bilionea ambaye anamiliki magari ya kifahari yakiwemo magari aina ya BMW, Mercedes, na mengine mengi.
Ramesh huyakodisha magari hayo kwa maelfu ya pesa kwa siku huku ada ya juu zaidi ikigharimu TSh 1,600,000/= Licha ya kuwa tajiri, Babu bado anaendelea na kazi yake ya kinyozi.
Kulingana naye maisha yake ya kale humkumbusha umbali alikotoka na kwa hivyo kumfanya kunyenyekea.
Babu huwasili kazini kwake huku akiendesha gari aina ya Rolls-Royce kwa wakati mwingine.
Safari yake ya kfanikiwa maishani ilikumbwa na changamoto kila mara hususan baada ya kumpoteza babayake akiwa na umri mdogo wa miaka saba.
Babu hakujua atakuwa bilionea atakapotimiza miaka 40 kupitia duka hilo la babake, kwani kwake ilikuwa kama ndoto.
Tajiri huyo alisema walikuwa wakishindia chakula kimoja kwa siku na mamake aliaga dunia baada ya kifo cha babayake.
Majukumu yalikuwa yamemuweka kwenye njia panda huku akipata ugumu wa kuchagua kati ya masomo na jinsi ya kujipatia mapato.
Bilionea huyo alidokeza kuwa ndoto yake ya kutaka kumiliki gari ilimsukuma kununua gari hilo la Maruti ambalo alianza kulikodisha.
Hamu yake ya magari iligeuka kuwa biashara ya mabilioni ya pesa ambayo inachangia pakubwa katika utalii nchini humo kwani magari yake hutumiwa kila mara na watalii.

Na Fatma Pembe.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KUTANA NA KINYOZI BILIONEA ANAE ENDESHA ROLLS-ROYCE, BMW AKIENDA KAZINI
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
8/10/2019 06:03:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: