Loading...

UTURUKI YAKAMILISHA KUTENGENEZA GARI LAKE LA KWANZA LINALOPAA

Loading...
Uturuki  yakamilisha kutengeneza gari lake la kwanza linalo paa angani, mfano wa gari hilo ambalo linajulikana kama "CEZERİ" umekwisha andaliwa.

Selçuk Bayraktar, meneja mkuu wa ufundi wa Baykar (CTO) na  rais wa wajumbe wa heshima wa taasisi ya teknolojia ya Uturuki (T3 Vakfi) ametangaza kwamba Uturuki itakuwa na gari lake la kwanza linalopaa angani.

Bayraktar aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter na mradi huo wa taifa wa gari linalopaa ujulikanao kama "CEZERİ". Alisema kwamba mfano “prototype” ya gari hilo umekamilika kutengenezwa na litaonyeshwa jinsi linavyopaa katika maonyesho ya teknolojia ya TEKNOFEST.
Na Mary Mkeu.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UTURUKI YAKAMILISHA KUTENGENEZA GARI LAKE LA KWANZA LINALOPAA UTURUKI YAKAMILISHA KUTENGENEZA GARI LAKE LA KWANZA LINALOPAA Reviewed by GEOFREY MASHEL on 8/10/2019 06:19:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.