Loading...
Rais wa Tanzania, John Magufuli Alhamisi Agosti Mosi, 2019 amepiga ‘push-up’ tisa kabla ya kuzindua jengo jipya la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015, ilikuwa ni kawaida kumshuhudia Rais Magufuli akipiga ‘push-up’ katika mikutano yake mbalimbali hali iliyotafsiriwa kuwa yuko imara kuwatumikia Watanzania.
Jana amerudia tena wakati akiongoza viongozi walioketi meza kuu kwenda kuwatunza waimbaji wa bendi ya Tanzania One Theatre (TOT).
Alipofika mbele ya wanenguaji wa bendi hiyo alisimama mbele yao kupiga ‘push-up’ tisa na kunyanyuka hali iliyoibua shangwe kwa waliohudhuria uzinduzi huo.
Imeelezwa, uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere umeongeza idadi ya abiria watakaokuwa wakihudumiwa na Uwanja huo kutoka abiria milioni 2 mpaka abiria milioni 8 kwa mwaka.
Ongezeko hilo limetokana na kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa Jengo la Tatu la Abiria katika Uwanja huo lenye uwezo wa kuhudumia abiria milioni 6 kwa mwaka.

Na Paskali Joseph.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RAIS MAGUFULI APIGA 'PUSH-UP' TENA UZINDUZI WA TERMINAL 3
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
8/02/2019 08:46:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: