Loading...
Makama moja nchini China Jumatatu imemhukumu kifungo cha miaka 12 jela mwanaharakati wa siku nyingi wa haki za binadamu anayefahamika kwa kuendesha tovuti inayofuatilia madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Taarifa ya mahakama ya jimbo la Sichuan imesema Huang Qi ametiwa hatiani kwa kuvujisha kwa makusudi siri za taifa na kuzitoa nje ya China jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Kupitia tovuti yake iitwayo 'Tianwang', mwanaharakati huyo amekuwa akijaribu kutoa msaada kwa wale wanaotafuta haki ikiwemo kesi za watu waliohamishwa kwa nguvu kutoka kwenye makaazi yao.
Kwenye hukumu hiyo, Huang ambaye umri wake ni wa kati kati ya miaka 50 pia ameondolewa haki zake zote za kisiasa kwa miaka 4.
Mwanaharakati huyo amekuwa kizuizi tangu mwaka 2016, hatua amabye ilizusha wasiwasi kutoka makundi ya haki za biandamu, Umoja wa Mataifa na mama yake mzazi.

Na Fatma Pembe.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
CHINA: MWANAHARAKATI WA SIKU NYINGI AHUKUMIWA MIAKA 12 JELA
Reviewed by By News Reporter
on
7/30/2019 08:12:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: