Loading...

WAKAZI WA KIGOMA WATISHIKA NA EBOLA, WATOA OMBI HILI KWA SERIKALI

Loading...
Wakazi wa Kijiji cha Mnanila Wilaya ya Buhigwe, mkoani Kigoma ambao wanapakana na nchi jirani ya Burundi, wameiomba Serikali kuongeza udhibiti wa njia zisizo rasmi zinazotumiwa na baadhi ya wananchi wa nchi jirani kuingia Tanzania, ili kuepuka ugonjwa wa Ebola.

Wananchi hao wamesema hayo wakati wa zoezi la utayari kwa vitendo kwa wahudumu wa dharura kwa wagonjwa wa Ebola, katika Hospitali ya Waadiventista wasabato ya Heri, ambapo wamedai kuna njia zisizo rasmi za kuingia nchini ambapo zisipodhibitiwa kuna uwezekano Ebola ikaingia nchini.

Kwa upande wake Mtendaji wa Kijiji cha Mnanila, Nuhu Lubanguka, ameiomba Serikali kutumia mikutano ya Vijiji kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na ugonjwa wa Ebola.

Kwa upande wake Mratibu wa Vituo vya Afya mipakani kutoka Wizara ya Afya, Remidius Kakulu, amesema Serikali imeendelea kuimarisha mifumo ya udhibiti, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanakuwa na elimu sahihi.
Na Timoth Samwel.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WAKAZI WA KIGOMA WATISHIKA NA EBOLA, WATOA OMBI HILI KWA SERIKALI WAKAZI WA KIGOMA WATISHIKA NA EBOLA, WATOA OMBI HILI KWA SERIKALI Reviewed by By News Reporter on 8/08/2019 08:01:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.