Loading...

Rais Museveni - "Nampenda Trump kwasababu anasema ukweli na uwazi juu ya Afrika"

Loading...
Kushoto rais Museveni, kulia rais Trump
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema anampenda rais wa Marekani Donald Trump katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa bunge la Afrika Mashariki jijini Kampala.
Museveni alisema Marekani ina rais mzuri sana wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa bunge la Afrka mashariki.
''Ninampenda trump kwasababu anasema ukweli mtupu, waafrika wanatakiwa kusuhisha matatizo yao wenyewe, Waafrika ni dhaifu sana'' Museveni.
Pongezi hizo za museven kwa Trump zinakuja saa chache tuu baada ya balozi wa Uganda kwa Marekani Deborah Malac kumkosoa Trump.
''Kauli zake zinachukiza na kukera sana'' amesema Deborah.

Rais Museveni Alivyotweet katika mtandao huo wa twitter 
Museveni alisema: "Rais Trump alisema ukweli aliongea juu ya Afrika. Waafrika wanapaswa kutatua matatizo yao. Hatuweza kuendelea kama ni wadhaifu. Ni kosa kujiona wenyewe ni dhaifu. Sisi ni mara 12 zaidi ya ukubwa wa nchi ya India, lakini kwanini sio imara?"

Hiyo ni kuonyesha nia ya dhati kabisa ameungana na kauli alizosema rais wa Marekani kwa kile kilichopigwa vita na baadhi ya viongozi wengi wa Afrika.
Rais Museveni - "Nampenda Trump kwasababu anasema ukweli na uwazi juu ya Afrika" Rais Museveni - "Nampenda Trump kwasababu anasema ukweli na uwazi juu ya Afrika" Reviewed by By News Reporter on 1/26/2018 08:57:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.