Loading...

SHAMBULIO KABUL: TALIBAN YAUA 59 KATIKA SHAMBULIO LA KUJITOA MUHANGA

Loading...
Majeruhi wa Shambulio la Kabul na wana mgambo wa Taliban nchini Afghanistan
Maafa katika shambulio hilo
Utawala nchini Afghanistan, umeituhumu Pakistan kwa kuwaunga mkono wanamgambo ambao walisababisha vifo vya zaidi ya watu 95 katika mlipuko wa bomu wa kujitoa mhanga mjini Kabul.
Watu 158 wamejeruhiwa.
Chanzo kinasema kwamba, shambulio hilo la jana Jumamosi, lililotekelezwa na kundi moja la wapiganaji la Haqqani, lililo na uhusiano mkubwa na lile la Taliban, na kuungwa mkono na Pakistan.

Utawala wa Afghanistan, sasa unaeleza kuwa shambulio hilo ni la kiwango cha mauwaji makubwa ya halaiki, dhidi ya binadamu.
Siku zote Islamabad imekanusha madai ya aina yoyote ya kuyaunga mkono makundi ya wanamgambo yenye nia ya kuhujumu utawala wa Afghanistan.
Gari moja la dharura la kuwahudumia wagonjwa, ambalo lilikuwa limejazwa vilipuzi, lililipuka katika kituo cha usalama barabarani baada ya kusimamishwa na askari, katika Wilaya ya Jiji Kuu Kabuli kulikokuwa na idadi kubwa ya watu.
Kwa njia ya taarifa, Rais wa Marekani Donald Trump, amelaani shambulio hilo, huku akitoa wito wa mbinu muafaka wa kupambana na kundi la Taliban.
Shambulio la sasa limetokea wiki moja tu baada ya Hoteli ya Intercontinental mjini Kabul kushambuliwa na watu zaidi ya 20 wakauwawa.
SHAMBULIO KABUL: TALIBAN YAUA 59 KATIKA SHAMBULIO LA KUJITOA MUHANGA SHAMBULIO KABUL: TALIBAN YAUA 59 KATIKA SHAMBULIO LA KUJITOA MUHANGA Reviewed by By News Reporter on 1/28/2018 10:03:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.