Loading...

URUSI YASHAMBULIA NA KUTEKA MELI ZA KIVITA ZA UKRAINE

Loading...
Urusi imezishambulia na kuziteka meli tatu za kivita za Ukraine zilizokuwa baharini katika rasi ya Crimea katika kisa ambacho kimezidisha uhasama baina ya mataifa hayo mawili.

Meli mbili ndogo za kivita, pamoja na meli moja ya kusindikiza meli ndizo zilizotekwa na wanajeshi wa Urusi.

Wahudumu kadha wa meli za Ukraine wamejeruhiwa.

Kila taifa linamlaumu mwenzake kwa kusababisha kisa hicho.

Leo Jumatatu, wabunge wa Ukraine wanatarajiwa kupiga kura kuidhinisha kuanza kutekelezwa kwa sheria za kijeshi.

Mzozo wa sasa ulianza pale Urusi ilipoituhumu Ukraine kwa kuingiza meli katika maeneo yake ya bahari kinyume cha sheria.

Urusi kisha iliweka meli kubwa ya kusafirisha mizigo na kuziba daraja la kuingia kwenye mlango wa bahari wa Kerch, njia pekee ya kuingia kwenye Bahari ya Azov na ambayo hutumiwa na mataifa yote mawili.

Wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Usalama na Ulinzi la Ukraine, Rais Petro Poroshenko alieleza vitendo vya Urusi kuwa "uchokozi usio na sababu na za kiwendawazimu."

Urusi imeomba kuandaliwe mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, mkutano ambao balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley amesema umepangiwa kufanyika saa tano asubuhi saa za New York (16:00 GMT) leo Jumatatu.
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
URUSI YASHAMBULIA NA KUTEKA MELI ZA KIVITA ZA UKRAINE URUSI YASHAMBULIA NA KUTEKA MELI ZA KIVITA ZA UKRAINE Reviewed by By News Reporter on 11/26/2018 07:33:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.