Loading...

WANAOWAPA MIMBA, KUOA WANAFUNZI ADHABU YAONGEZEKA

Loading...
SERIKALI imesema imebadili utaratibu gerezani kwa watu watakaotumikia kifungo cha miaka 30 jela kutokana na kuwapa mimba au kuoa mwanafunzi.

Utaratibu huo uliobadilishwa ni wa kuhesabu siku, ambapo sasa mfungwa wa makosa hayo atahesabiwa usiku na mchana kuwa ni siku moja badala ya usiku na mchana kuwa siku mbili ilivyo kwa wafungwa wengine.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ndiye aliyefichua suala hilo jijini hapa jana, alipozindua Kampeni ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10.

Kampeni hiyo imeratibiwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Majaliwa pia aliwataka wadau kutumia siku hizo kuwasilisha mapendekezo kama kuna upungufu unaohitaji sheria zitungwe kuwasilisha kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya kutunga sheria.

Takwimu za mwaka 2016 zinaonyesha asilimia 40 ya wanawake wenye umri wa miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili.
Na Neema Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WANAOWAPA MIMBA, KUOA WANAFUNZI ADHABU YAONGEZEKA WANAOWAPA MIMBA, KUOA WANAFUNZI ADHABU YAONGEZEKA Reviewed by By News Reporter on 11/26/2018 08:35:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.