Mwimbaji nyota katika muziki wa bongo fleva, Diamond Platinumz a.k.a Simba ametangaza rasmi ndoa kati yake na mpenzi wake mpya, ambaye ni mwanamitindo wa Mkenya na mtangazaji wa radio, Tanasha Donna Oketch.
Diamond, ambaye alionekana katika umma kwa mara ya kwanza akiwa na mrembo huyo Mkenya juma lililokwisha katika tamasha la Thika alilovunja rekodi ya mauzo, pia amefunguka na kusema yupo tayari kutulia na kuoa baada ya kutembea na wasichana kadhaa huku na kule.
Akimuelezea mrembo Tanasha Diamond alisema:
"Tanasha Oketch ni mwanamke pekee ambaye amechukulia uzito matamanio yangu ya kutaka kuwa na mke. Na, kutokana na kujidhatiti kwake juu yangu, Natangaza rasmi, kwamba yeye ndi
Loading...
e nitakayemuoa,"
Aliongezea:
"Ni yeye pekee ambaye anavigezo ninavyo vitaka ili mwanamke awe mkwe wangu. Ijapokuwa wengine huangalia vigezo kama sura nzuri, maumbile na mwendo.
"Hakuna mwanamke yeyote mbele ya macho yangu - sasa au zamani - ninaweza kumfananisha na Tanasha kuanzia uzuri wa sura, maumbile na tabia za Tanasha,"
Diamond aliweka wazi kuwa alikutana na familia ya Tanasha wakati alipotembelea Kenya.
Na Mary Mkeu.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
DIAMOND ATANGAZA NDOA KWA MPENZI WAKE MKENYA
Reviewed by By News Reporter
on
12/06/2018 09:50:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: