Loading...

QUEEN DARLEEN: WATANZANIA WANAPENDA SANA MAPENZI KULIKO KULA

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Queen Darleen ameibuka na kuweka wazi sababu za kupendelea kuimba nyimbo za mapenzi.

Queen Darleen amesema anapenda sana kuimba nyimbo za mapenzi kwa sababu Watanzania wanapenda sana mapenzi kuliko kula kwaiyo nyimbo za mapenzi zimekuwa na soko zaidi Bongo.

Queen Darleen ameweka wazi kuwa wasanii wengi bongo soko lao lipo kwenye nyimbo za mapenzi ndio maana hata ukiangalia nyim
Loading...
o hizo ndizo zinafanya vizuri zaidi.

"Unajua Watanzania wanapenda sana Mapenzi kuliko kula kuliko hata kufanya kazi ndio maana nyimbo za mapenzi zinafanya vizuri zaidi kwenye Bongo fleva na ndio maana wakina Mbosso, Lavalva wanafanya vizuri na Diamond Mpaka leo yupo kwenye chati kisa nyimbo za mapenzi ," alisema mrembo huyo na dada wa mwanamuziki Diamond.

Queen alidai anatamani Label ya WCB isaini msanii wa kike ili yeye apate chagamoto ya kufanya kazi nzuri zaidi.
Na Neema Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
QUEEN DARLEEN: WATANZANIA WANAPENDA SANA MAPENZI KULIKO KULA QUEEN DARLEEN: WATANZANIA WANAPENDA SANA MAPENZI KULIKO KULA Reviewed by By News Reporter on 12/06/2018 11:21:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.