Loading...

UBAKAJI DAR NI TISHIO, VISA 714 VYARIPOTIWA

Loading...
RIPOTI ya vitendo vya ubakaji vilivyoripotiwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa miezi 10 ya mwazo ya mwaka huu inabainisha kuwa jumla ya wanawake na watoto 714 wamebakwa katika kipindi hicho.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alitoa takwimu hizo jana jijini wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto Mkoa wa Dar es Salaam.
"Kesi za kulawiti zilizoripotiwa ni 229, zilizopo chini ya upelelezi 186, zilizopo mahakamani ni 43 zikiwa na jumla ya watuhumiwa 47," alisema.

Kamanda Mambosasa alisema kuna changamoto ya jamii kutotambua haki za binadamu huku akisisitiza inahitaji kushughulikiwa na jamii.

"Tunaamini elimu ambayo inazidi kutolewa na askari katika madawati mbalimbali ya ukatili wa kijinsia yaliyoanzishwa katika mikoa yetu ya kipolisi na wilaya zetu za kipolisi itasaidia," alisema.

Alisema katika kukabiliana na changamoto hiyo, wataendelea kuwasaka wanaofanya vitendo hivyo na kuwafikisha mahakamani bila huruma.
Na Catherine Kisese.


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UBAKAJI DAR NI TISHIO, VISA 714 VYARIPOTIWA UBAKAJI DAR NI TISHIO, VISA 714 VYARIPOTIWA Reviewed by By News Reporter on 12/01/2018 10:05:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.