Loading...

MASHINDANO YA UREMBO WA NGAMIA SAUDI ARABIA YATUMBUKIA KATIKA KASHFA NZITO

Loading...
Ngamia 12 wamepoteza sifa za mashindano ya urembo nchini Saudi Arabia baada ya wamiliki wao kuwachoma sindano ya kubadili maumbile.

Maelfu ya ngamia wameshirikiswa katika tamasha la Mfalme Abdulaziz na kushindanishwa kwa muonekano wa nyuso zao, nundu na maumbile yao.

Lakini majaji waliingilia kati wakati walipogundua kwamba baadhi ya udanganyifu ulifanyika na baadhi ya wamiliki waliotaka kushinda tuzo za fedha.
Vile vile tamasha hilo lina mashindano ya riadha ya ngamia na kuonja maziwa, lina tuzo ya fedha taslim dola milioni 57.
Mtandao wa habari wa The National imeripoti kuwa Ali Al Mazrouei, mwana wa mfugaji bingwa , alisema dawa ya botox ilitumika kwenye midomo, pua na hata taya.
"Dawa hiyo inavimbisha kichwa kwa hio ukimuona ngamia unadhani ana kichwa,mdomo na pua kubwa" aliezea Mazrouei.
Majaji pia walikuwa wakishindanisha nundu na misuli ya ngamia.
Kabla ya tamasha hilo, vyombo vya habari vya Saudia viliripoti daktari wa wanyama alikamatwa akiwafanyia operesheni ngamia hao ili kuwabadilisha ukubwa wa masikio pamoja na kuwachoma sindano ya dawa ya kubadilisha maumbile.
MASHINDANO YA UREMBO WA NGAMIA SAUDI ARABIA YATUMBUKIA KATIKA KASHFA NZITO MASHINDANO YA UREMBO WA NGAMIA SAUDI ARABIA YATUMBUKIA KATIKA KASHFA NZITO Reviewed by By News Reporter on 1/31/2018 09:33:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.