Loading...

BREAKING NEWS: RAIS JACOB ZUMA AJIUZULU

Loading...
Rais Jacob Zuma ametangaza kujiuzulu leo jioni, baada kutakiwa afanye hivyo na uongozi wa chama chake cha ANC. Kiongozi wa chama chake hicho bwana Maphorisa ambaye pia ni makamo wa rais wa nchi alimtaka rais Zuma ajiuzulu mara kufuatiwa na kashfa zinazomkabili za rushwa na kusema kama angekaidi matakwa hayo bunge lingempigia kura za kutokuwa na imani naye.

Ingawa rais Zuma alisema hakubaliani na matakwa hayo kwa kumlazimisha kujiuzulu mapema leo akizungumza na vyombo vya habari. Na kudai amewapigania wananchi kwa nguvu zake zote na haoni haja ya kufanya hivyo.

Zuma aliingia katika utawala tangu mwaka 2009, na amekuwa na kashfa kadhaa za rushwa na kuperekea wananchi na wanasiasa kupoteza imani naye.
BREAKING NEWS: RAIS JACOB ZUMA AJIUZULU BREAKING NEWS: RAIS JACOB ZUMA AJIUZULU Reviewed by By News Reporter on 2/15/2018 12:35:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.