Loading...

DAKTARI AWAAMUKIZA WATU ZAIDI YA 40 VIRUSI VYA UKIMWI

Loading...
Angalau watu 40 wamekutwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI huko nchini India katika jimbo lililopo kaskazini mwa jiji la Utter Pradesh, ambapo Daktari asiyefuzu alidaiwa kutumia bomba moja la sindano kutibu wagonjwa wote katika kituo chake cha afya, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya eneo hilo.

Taarifa zilisambaa siku ya Jumatano, na ni miezi kadhaa baada ya watu kuathirika, wakiwemo watoto, waliogunduliwa katika kambi ya afya iliyoandaliwa na NGO mwezi Novemba mwaka jana katika mji wa Bangarmau Wilaya ya Unnao, ili ripotiwa na kituo cha habari cha Times Now New Channel.

"Kuna kesi zaidi ya arobaini [HIV] za walioambukizwa virusi vya ukimwi [Kati ya watu 400 waliofanyiwa vipimo],"  alisema Sunil Bangarmau mbunge wa eneo hilo akizungumza na waandishi wa habari.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Daktari huyo ameshachukuliwa hatua kali za kisheria na serikali inafanya mpango wa kufanya msako na kufungia vituo vyote vya afya visivyo na leseni.
DAKTARI AWAAMUKIZA WATU ZAIDI YA 40 VIRUSI VYA UKIMWI DAKTARI AWAAMUKIZA WATU ZAIDI YA 40 VIRUSI VYA UKIMWI Reviewed by By News Reporter on 2/06/2018 03:32:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.