Loading...
Mzee Kingunge enzi za Uhai wake. |
Familia imetangaza rasmi siku ya mazishi ya mwanasiasa mkongwe Mr. Kingunge Ngombale Mwiru. Mwili wa Kingunge unatarajiwa kwenda kupumzishwa siku ya jumatatu katika makuburi ya Kinondoni, taarifa ya familia imesema.
Akizungumza na vyombo vya habari jana Februari 2, Bw. Ally Mchumo msemaji wa familia alisema Kingunge ambaye alifariki leo katika hospitali ya Muhimbili atazikwa karibu na mkewe, Peras Kingunge.
Mke wa Kingunge alikufa Disemba 4, mwaka jana na alizikwa Januari 11 katika Makaburi ya Kinondoni. "Dini gani itatumika kuendesha shughuli ya mazishi yake itajulikana baadaye, kwa sasa umma unapaswa kujua kwamba atazikwa Jumatatu katika Makaburi ya Kinondoni," alisema.
Alisema kifo chake ni hasara kwa nchi, kwa sababu mchango wake uligusa maisha ya wengi ya Watanzania wakati akilihudumia taifa katika nyanja tofauti tofauti.
Mpwa wa Marehemu, Bw. Tony Mwiru alisema familia imeshtushwa na kifo cha baba yao huyo kwa sababu ameondoka mapema sana, kwa maana bado walikuwa wanamuhitaji kutokana na bado kuomboleza kifo cha Mama yao ambaye ni mke wa Marehemu.
"Wakati sisi bado tunaomboleza kifo cha mama yetu kipenzi, tumepoteza baba pia. Ni pigo kubwa kwetu na pengo kubwa katika familia yetu. Hata hivyo, ni Mungu ambaye anaamua kila jambo na hatuna haja ya kulalamika," alisema.
Mdogo wa Marehenu Bw. Enock Mwiru alisema kaka yake alikuwa muhimu sana katika kuiunganisha familia na mpatanishi pale familia inapotofautina.
Mkongwe huyo aliyefariki katika hospitali ya Muhimbili siku ya Ijumaa (Februari 2) saa 10 alfajiri ambapo alifikishwa hospitalini hapo kufuatia shambulio la kung'atwa na mbwa nyumbani kwake.
FAMILIA YATANGAZA RASMI SIKU YA MAZISHI YA MZEE KINGUNGE
Reviewed by By News Reporter
on
2/03/2018 10:34:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: