Loading...

KUFUATIA KIFO CHA MSANII MOWZEY RADIO MASWALI MENGI YAIBUKA

Loading...
De Bar ya Uganda Yalipofanyika mauaji ya msanii Mowzee yafungwa.
Almashauri ya Manispaa ya Entebbe imefunga baa ya De bar, kiwanja maarufu kwa kustarehe ambapo mlinzi mmoja iliripotiwa kumpiga na kumjeruhi vibaya mwimbaji Mowzey Radio aliyefariki alhamisi ya juzi katika hospitali ya Case.

Mowzey, pia anajulikana kama Moses Ssekibogo, ameripotiwa kuwa alikuwa anauguza jeraha la kichwa baada ya kupata mikwaruzo januari 22.

Katika barua iliyoandikwa tarehe 1 februari ilifikishwa kwa uongozi wa baa hiyo, Karani wa jiji la Entebbe bwana Dan Lutaya imepatia "nguvu manispaa inayosimamia biashara hiyo" kuifunga baa hiyo mara moja kutokana na tukio lililotoke.
Barua ya kufungwa baa hiyo:
Mowzey alifikishwa katika Kliniki ya hospitali ya Case  huko Kampala ambapo ilitangazwa amefariki dunia siku ya Alhamis asubuhi. Maelezo ya majeraha aliyopata kichwa yalikosa mashiko baada ya baadhi ya watu walidai aliyeyazua yote hayo ni Mowzey kwa kummwagia wiski meneja wa baa hiyo.

Aliripotiwa kupigizwa chini ya sakafu na mmoja wa mlinzi katika baa hiyo, na kupigiza kichwa chake chini na kusababisha damu kuvuja katika ubongo.

Manispaa pia imeifutia leseni baa hiyo, na Lutaya amesisitiza ikionekana imefunguliwa baa hiyo kwa kukaidi agizi hatua kari za kisheria zitachukuliwa.

Polisi wa Uganda pia wamethibitisha kuwa mlinzi wa baa hiyo anakabiliwa na kesi ya 'mauaji ya kukusudia' na sio tena 'shambulio la kujeruhi mwili'.

Je! mfululizo huu wa mauaji ya wasanii, nini kiini?

Tukio hilo la wiki iliyopita sawa na lile lililosababisha kifo cha AK47 mwaka 2015.

Emmanuel Mayanja Hummertone aka AK47 alipigwa katika baa, Kabalagala kubla ya kufa wakati wa kuwasili hospitali ya Nsambya, iliripotiwa kuwa fuvu la kichwa chake limevunjika.

Mwanamuziki alitokea katika familia ya kimuziki ambayo inajumuisha kaka yake Joseph Mayanja aka Jose Chameleone, Pius Mayanja aka Pallaso na  Douglas Mayanja aka Weasle.

Ripoti ilieleza kuwa AK47 alipigwa katika baa kwanza na akaenda katika chumba cha kujisafisha, ambapo ilifikiriwa kuwa alitereza na kuanguka.

Baa hiyo ya DEJAVU, ilikuwa inamilikiwa na Jeff Kiwanuka, meneja wa zamani wa wasanii Radio and Weasle.

Pia, Octoba mwaka jana, mtengenezaji na mtayarishaji wa nyimbo Dau Muto aka Danz Kumapeesa alifariki miezi minne baada kuuguzwa kitandani kwa muda mrefu katika hospitali ya Nsambya.

Mtayarishaji wa muziki huyo iliripotiwa kulazwa hospitalini baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana, ambao walimkaba na kumpiga usiku mnene June mwaka jana.

Polisi wa Uganda wameshaanza kuchukua hatua zaidi za kiusalama kuchunguza mauaji haya kwa kina kwakuwa huwenda ni mauaji yanayopangwa na watu fulani.
KUFUATIA KIFO CHA MSANII MOWZEY RADIO MASWALI MENGI YAIBUKA KUFUATIA KIFO CHA MSANII MOWZEY RADIO MASWALI MENGI YAIBUKA Reviewed by By News Reporter on 2/03/2018 09:13:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.