Loading...

HUYU NDIYE MWANAUME ALIYESHINDA MASHINDANO YA ULIMBWENDE

Loading...
Kushoto ni akiwa kama mrembo Arina Alieva, kulia akiwa kama Ilay Dyagilev.
Ilay Dyagilev (23), huko Kazakhistan amezua hali ya sintofahamu baada kushinda mashindo ya ulimbwende yaliyoendeshwa kwa njia ya mtandao hali ya kuwa yeye ni mwanaume na sio 'Arina Alieva' kama ilivyotajwa hapo mwanzo katika shindano hilo.

Arina Alieva alishinda shindano hilo kwa jumla ya kura 2,012 kwa kumshinda muhasimu wake Aikerim aliyeambulia kura 1,975, Arina alipita katika mchujo wa hatua ya nusu fainali kwa kuwa nafasi ya 16 kati ya washindani 142.

Taarifa zinasema, majaji wa shindano hilo waliamua kumpokonya Arina ushindi huo baada ya kuthibitisha kuwa yeye sio mwanamke na jina lake kamili anaitwa 'Ilay Dyagilev' na kutuma picha kwa ushahidi , na badala yake ushindi walimtunuku aliyemfuatia kwa kura.

Ila mpaka sasa wapiga kura wa shindano hawaamini kuwa mshindi huyo ni mwanaume na sio mwanamke ijapokuwa na ulimbwende wote ule aliouonyesha katika mitandao.
HUYU NDIYE MWANAUME ALIYESHINDA MASHINDANO YA ULIMBWENDE HUYU NDIYE MWANAUME ALIYESHINDA MASHINDANO YA ULIMBWENDE Reviewed by By News Reporter on 2/09/2018 07:42:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.