Loading...
Zaidi ya watoto 300 waliokuwa wanatumikishwa kama wanajeshi wameachiwa kutoka jimboni Yambio nchini Sudan
Kusini chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuwasaidia watoto hao kurejea kwenye jamii.
Kati ya watoto 311 walioachiwa na makundi ya waasi, 87 kati yao ni wasichana, imesema taarifa ya tume ya
umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS.
Mjumbe wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini David Shearer, amesema hii ni mara ya kwanza
kwa wasichana wengi zaidi kuachiwa na makundi ya waasi.
Wanaharakati wa haki za binadamu wamepongeza hatua hii na kusema kuwa watoto hao walikua hawatendewi haki
kwa kutumikishwa kama wanajeshi wakati ambapo umri wao hauwaruhusu.
Tabia hii imekua sugu barani Afrika hasa katika nchi zinazokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Masharika mbalimbali ya haki za watoto yamekua yakikemea hali hii, huku yakiomba hatua kali zichukuliwe kwa
kukomesha tabia hii.
ZAIDI YA WATOTO 300 WAACHIWA HURU NA MAKUNDI YA WAASI SUDAN
Reviewed by By News Reporter
on
2/09/2018 06:42:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: