Loading...

IMEGUNDULIKA ALAMA ZA VIDOLE ZINAUWEZO WA KUGUNDUA MAGONJWA YA KISUKARI, KANSA NA PUMU

Loading...
Alama za vidole, tumezoea zikitumika kukamata waalifu, kumbe pia husaidia kuchunguza watu ambao wapo katika hatari ya magonjwa fulani fulani hata kabla ya dalili za mwanzo kuonekana.

Tafiti mpya zinaonyesha kwamba wanawake wenye aina maalum ya alama za vidole - wametajwa wenye mzunguko mdogo na mikunjo mingi wanahatari kubwa ya kuugua kansa.

Hapo nyuma, watafiti waligundua kuna uhusiano kati ya alama za vidole na alama za viganja katika kuonyesha dalili za magonjwa kama Kisukari, Kupoteza Kumbu kumbu, Leukemia, Msongo wa mawazo, na Magonjwa ya fizi.

Nadharia iliyonyuma ya tafiti hiyo ya kisayansi inayoonyesha uhusiano kati ya alama za vidole na hatari ya magonjwa - ni kwamba kama ukuaji wa mikono na miguu, viungo au tishu mwanzoni mwa maisha ya kijusi, basi kutakuwa na mabadiliko ya wa mpangilio wa alama za vidole au viganja.

Kwahiyo Magonjwa ya kansa, Kisukari, Vizi na Pumu yanaweza kugundulika mapema kwa kuangalia mpangilio wa alama za vidole na viganja vya muathirika.
IMEGUNDULIKA ALAMA ZA VIDOLE ZINAUWEZO WA KUGUNDUA MAGONJWA YA KISUKARI, KANSA NA PUMU IMEGUNDULIKA ALAMA ZA VIDOLE ZINAUWEZO WA KUGUNDUA MAGONJWA YA KISUKARI, KANSA NA PUMU Reviewed by By News Reporter on 2/13/2018 07:58:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.