Loading...
Mchungaji Mkuu amekamatwa kwa kuwapa ujauzito mabinti wawili wenye umri chini ya miaka 18 nchini Kenya.
Alfred Maingi Ndolo (30), mchungaji mkuu katika kanisa la Unabii nchini Kenya, anashikiliwa na polisi baada ya kushukiwa kuwapa ujauzito watoto wa kike yatima wenye umri wa miaka 15 na 17, watoto hao walifunguka na kusema walikuwa wanamahusiano ya kimapenzi na mchungaji huyo na sasa wanaujauzito.
Kenyan News Agency iliripoti kwamba bibi wa watoto hao aliyekuwa akiishi nao, aliripoti swala hilo kwa polisi na mshukiwa alikamatwa na uchunguzi zaidi unaendelea. Bibi yao alidai mchungaji alikuwa akiwatembelea mara kwa mara nyumbani hapo na alikuwa mshauri wa kiroho wa mabinti hao, lakini alitumia kigezo hicho na kuanza kuwaingilia ki mwili.
Bibi alisema: "Sikuweza kuhisi chochote mpaka mapema wiki nilipoanza kuona hali ya kiafya ya binti mjukuu wangu wa miaka 15 kubadilika na kuamua kuwapereka wote hospitali kwa ajili ya vipimo na nikaambia wote wanaujauzito tayari."
Ripoti inasema kinachosubiriwa ni vipimo vya vinasaba kuhakiki kama mimba za mabinti hao ni zimehusika na mchungaji huyo basi atafikishwa mahakamani na afungwe jela kwa ubakaji.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika Mashariki punde zinapojiri.
MCHUNGAJI AKAMATWA KWA KUWAPA UJAUZITO WATOTO WAWILI
Reviewed by By News Reporter
on
2/23/2018 07:44:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: