Loading...

MISS RWANDA 2018: HAWA NDIO WAREMBO WATAKAOSHIRIKI FAINALI ZA KUTWAA TAJI LA UREMBO

Loading...
Washindi 20, katika fainali za uchaguzi wa awali.
Mbio za kinyang'anyiro cha kutwaa taji la urembo nchini Rwanda zimezidi kushika kasi baada kupatikana washindi 20 wa awali watakaoshiriki katika fainali za kumpata mrembo atakayetwaa taji hilo. Warembo 35 walishiriki katika uchaguzi wa awali uliofanyika siku ya Jumamosi, warembo 15 kati yao walipigwa panga.

Washindi hao 20 waliobahatika kuvuka katika hatua ya uchaguzi wa awali ndio watakaoshindania kuwania taji la Mrembo wa Rwanda Februari 24 mjini Kigali katika ukumbi wa Kigali Convention Center (KCC).

Katika Ukumbi wa PSF Expo huko Gikondo ambapo fainali za uchaguzi wa awali zilifanyika hali ya majonzi na furaha ilitawala katika nyuso za warembo hao, na kwa wale walioanguka walijisikia vibaya ila kwa wale waliobahatika kupita katika hatua ya fainali walitawaliwa na furaha.

Kati ya washiriki 20 waliovuka katika hatua ya fainali, kanda ya Magharibi ndio wanawakilishwa na warembo wachache kuliko wote mwaka huu kwa kupereka washiriki wawili tu ambao ni Liliane Iradukunda, na Fiona Uwase.

Kanda wa Kusini ndio wanawashiriki wengi zaidi kwenye kambi za fainali hizo kwa kuwakilishwa na warembo tisa (9). Ikiwa Kigali inawawakilishi watatu, na Kanda ya Mashariki inawashiri sita (6).

ZIFUATAZO NI PICHA ZA WAREMBO HAO WATAKAOSHIRIKI KATIKA FAINALI ZA MREMBO WA RWANDA:
 
 

MISS RWANDA 2018: HAWA NDIO WAREMBO WATAKAOSHIRIKI FAINALI ZA KUTWAA TAJI LA UREMBO MISS RWANDA 2018: HAWA NDIO WAREMBO WATAKAOSHIRIKI FAINALI ZA KUTWAA TAJI LA UREMBO Reviewed by By News Reporter on 2/07/2018 02:08:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.