Loading...
Filamu ya Kiafrika Kusini kwa jina INXEBA iliyozinduliwa Agosti 16, mwaka jana sasa inarushwa katika mtandao wa Netflix.
Inxeba ndio filamu pekee ya Afrika Kusini ambayo inaonyeshwa katika mtandao wa Netflix.
Filamu hiyo ya kusisimua inayosimulia simulizi ya Xolani na wanaume wenzake katika jamii Xhosa walifunga safari na kuelekea mlimani na kundi la wavulana ili wakawatahiri, ijapokuwa mmoja wa watahiriwa hao aligundua siri yake iliyojificha.
Waafrika Kusini wavuka boda zaidi katika soko la filamu kwa kuweza kufanikisha filamu ya ya Inxeba, The Wound, kuonyeshwa katika mtandao wa Netflix maarufu kwa kuonyesha filamu mashuhuri duniani.
Kufuatia uzinduzi wa filamu hiyo huko Afrika ya Kusini Februari 2, katika majumba ya Sinema kuna watu kadhaa wamenza kuisema vibaya, kwamba inaelezea utamaduni wa kabila la Xhosa katika picha mbaya na hata kuperekea filamu hiyo kufanya vibaya katika soko la ndani.
Lakini Mtayarishaji wa filamu hiyo, John Trengove alisema: "Kila mtu anahaki ya kuizungumzia filamu hii lakini linapokuja swala la kuifungia, tunajua ni chuki binafsi tu za watu."
INXEBA, THE WOUND FILAMU YA KWANZA YA KIAFRIKA KUSINI KUONYESHWA NETFLIX
Reviewed by By News Reporter
on
2/07/2018 05:15:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: