Mchekeshaji maarufu wa nchini Uingereza, Rowan Atkinson a.k.a Mr. Bean amerudi tena kwa kuachia muendelezo wa filamu yake ya 'Johnny English Strikes Again' ambaye ameigiza kama mpelelezi wa Kiingereza aliyejaribu kufanya upelelezi wa makosa ya kimtandao na kusababisha huaribifu na maafa mengi sana katika hiki kionjo chake kipya.
Hii imekuja baada ya miaka 7 kupita tangu alipozindua filamu yake kama hii mwaka 2011 ya 'Johnny English Reborn', filamu ya kuchekesha yenye muendelezo. Filamu hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi 5 Oktoba, 2018 kwa Uingereza na Marekani 26 Oktoba, 2018.
Loading...
if;">
Filamu hii ya kuchekesha iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu, pia imemshirikisha Emma Thompson ambaye ameigiza kama Waziri mkuu wa Uingereza ambaye, alishangazwa na Johnny kukosa ujuzi wa upelelezi kama wenzake.
Vioja na vituko alivyofanya Mr. Bean katika filamu hiyo basi sio ya kukosa baada ya kuzinduliwa.
Na Haika Gabriel.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MOVIE LEO: MCHEKESHAJI MR. BEAN KUJA NA 'JOHNNY ENGLISH STRIKE AGAIN'
Reviewed by By News Reporter
on
8/30/2018 03:03:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: