Loading...

WAZIRI NCHEMBA ATEKETEZA EKARI SITA (6) ZA BANGI

Loading...
Mhe. Mwiguli Nchemba akiwa pamoja na Maskari waliofanikisha kuchoma shamba hilo

Mhe. Mwigulu alipokuwa akiwasha shamba hilo la bangi.
Waziri wa mambo ya ndani nchini, Mwigulu Nchemba leo ameongoza oparesheni ya kuteketeza jumla ya ekari  sita za bangi zilizokuwa zimelimwa katikati ya msitu ndani ya kijiji cha Engalaoni wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Mwigulu akishirikiana na kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha,(RPC) Charles Mkumbo pamoja na vikosi vya askari wa jeshi la polisi mkoani hapa walilazimika kuacha magari yao njiani na kutembea umbali wa kilomita 5 milimani kufika katikati ya msitu huo ambapo wamiliki wa mashamba hayo walitokomea kusikojulikana.

Akizungumza na waandishi wa habari  wakati wa zoezi hilo Mwigulu alisema kwamba serikali itaendelea na oparesheni pande zote za nchi na haitasita kuwakamata wahusika wote na kutaifisha magari yatakayotumika kusafirisha bangi.

Akizungumza na askari waliokuwa wakishiriki katika zoezi hilo Mwigulu mbali na kuwapongeza kwa kazi wanayofanya lakini aliwambia kwamba pamoja na kufanikiwa kuteketeza madawa ya kulevya yanayolimwa mashambani lakini waongeze juhudi pia katika kupambana na madawa ya kulevya yanayotengenezwa viwandani.
WAZIRI NCHEMBA ATEKETEZA EKARI SITA (6) ZA BANGI WAZIRI NCHEMBA ATEKETEZA EKARI SITA (6) ZA BANGI Reviewed by By News Reporter on 2/07/2018 12:30:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.