Loading...
Serikali ya Rwanda imepiga marufuku utoaji adhana, wito kwa waumini wa kiislamu kudiriki ibada ambao hutolewa mara tano kwa siku kwa madai kuwa wito huo huwa unawakera raia mjini Kigali.
Uamuzi huo umechukuliwa katika eneo la Nyarugenge, eneo ambalo kunapatikana miskiti mingi mjini Kigali.
Serikali inadai utoaji wa adhana unasababisha kelele nyingi na hivyo misikiti inatakiwa kutafuta njia nyingine ya kuwaita waumini wake.
Hata hivyo bado haijajulikana ni adhabu ipi misikiti itapatiwa endapo adhana zitaendelea kutolewa kama kawaida.
Mufti mkuu nchini Rwanda ameshangazwa sana na tangazo hilo na kusema kuwa suala hilo ni lazima lijadiliwe kwa kina.
Zaidi ya makanisa 800 yamefungiwa nchini Rwanda ndani ya siku chache zilizopita kwa madai ya kutokidhi vigezo na masharti.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kimataifa punde zinapojiri.
ADHANA KWA KUTUMIA VIPAZA SAUTI MISIKITINI YAPIGWA MARUFUKU - RWANDA
Reviewed by By News Reporter
on
3/16/2018 05:21:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: