Loading...

MUME WA ZAMANI WA FLORA MBASHA AIBUA MAPYA

Loading...
Aliyekuwa mume wa zamani wa mwimbaji wa nyimbo za injili Flora Mbasha amefunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram akidai apatiwi nafasi ya kuonana na mwanae kipenzi Lizy.

Emmanuel Mbasha alifunguka zaidi na kusema, lakini anamshukuru mzazi mwenzake huyo kwa kumzalia mtoto mzuri wa kike ambaye walimlea kwa muda wa miaka miwili tangu alipokuwa mdogo hadi walipoachana. Kwa sasa Flora ameolewa na Daudi Kusekwa kwa ndoa ya kanisani.

Akifunguka kupitia ukurasa wa instagram alisema: " “Ulinizalia mtoto mzuri sana kwa hilo nakushukuru mno. Nimemmiss Lizy sana unipe basi mtoto unaninyima kabisa daah karibu mwaka wa pili inaelekea wa tatu sasa sijamwona mtoto. Du, mimi baba yake tu ila nakuomba hata siku moja moja nifurahie maisha na dogo basi nakuomba nimwone mwanangu Lizy."

“Najua hata mtoto amenimiss sana, kwa mana ameondoka kwangu akiwa mkubwa na nimemlea tangu mtoto ila anashindwa kuongea tu, najua ananikumbuka sana.” 

“Mahakama iliamua mtoto akae na Mama ila niwe namwona, sasa unapingana na mahakama. Sitaki povu nimeongea na mzazi mwenzangu X wife, mke wa mtu.. njia za kawaida naona imeshindikana unakaza sana aise sasa inabidi nikuombe Insta tu,”

Kwa mujibu wa alichokisema kupitia instagram, Mbasha anahitaji waweke kando tofauti zao na pengine waangalie haki ya mtoto zaidi.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
MUME WA ZAMANI WA FLORA MBASHA AIBUA MAPYA MUME WA ZAMANI WA FLORA MBASHA AIBUA MAPYA Reviewed by By News Reporter on 3/11/2018 09:56:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.