Loading...

NEEMA KWA WAKINAMAMA WAJAWAZITO NCHINI

Loading...
BOHARI ya Dawa (MSD) imetangaza neema kwa kinamama wajawazito baada ya kuleta mfuko wenye vifaa vyote vya kujifungulia, lengo kuu likiwa ni kupunga vifo vya wakati wa uletaji kiumbe kipya duniani.

BOHARI ya Dawa (MSD) imetangaza neema kwa kinamama wajawazito baada ya kuleta mfuko wenye vifaa vyote vya kujifungulia, lengo kuu likiwa ni kupunga vifo vya wakati wa uletaji kiumbe kipya duniani.

Imeelezwa mfuko huo utajumuisha vifaa 12 ambavyo ni pamba kubwa, mpira wa kuzuia uchafu, taulo ya kike ya wazazi, sindano ya kuzia damu kupotea na mipira ya mkojo.

Vingine ni nyembe za kupasulia, kibana kitovu cha mtoto, dawa ya spiriti, Detol ya maji, sindano ya ganzi, mabomba ya sindano mawili na nyuzi za kushonea.

Mkurugenzi Mkuu MSD, Lauren Bwanakunu aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa za maboresho ya huduma ya MSD.

“Mfuko huo utauzwa kwa Sh. 21,000 tu katika maduka ya MSD," alisema Bwanakunu na kwamba "mtu yoyote anaruhusiwa kununua".

"Bei hiyo ni tofauti na maduka mengine yanayouza kuanzia Sh. 55,000 hadi 60,000.

“Na wananchi wanaohitaji kutoa vifaa hivi kama msada kwa wananchi au vituo vya kutolea huduma za afya nchini wanahimizwa kufika MSD kununua kwa bei hiyo nafuu.”

Bwanakunu alisema vifaa hivyo vya kuzalishia akina mama ni moja ya vifa muhimu vinavohitajika mama mjamzito awe navyo anapokwena kujifungua.

Alisema kati ya vifaa hivyo, kifaa cha mpira wa kuzuia uchafu ndio unaouzwa gharama zaidi kwa Sh. 13,000. Alisema mfuko huo hauingizi maji na unadumu kwa miaka mitano.

Wakati huo huo, Mkurugenzi Mkuu MSD, Lauren Bwanakunu amesema hali ya upatikanaji wa dawa muhimu zipatazo 135 umefikia asilimia 90.

Alisema upatikanaji wa dawa hizo muhimu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya umefikia asilimia 85 hadi 98.

Alisema upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi na za kutibu Malaria ni asilimia 100, wakati dawa za uzazi wa mpango ni asilimia 67, na dawa za kutibu kifua kikuu na ukoma ni asilimia 63.

Kuhusu deni la MSD wanalolidai Serikali, Bwanakunu alisema limefikia Sh.bilioni 142 lakini serikali iko katika mkakati wa kulilipa.

Kadhalika, Bwanakunu alisema MSD imeendelea kukidhi viwango vya ubora vya kimataifa katika mfumo wa ununuzi, utunzaji na usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara, na kupata ithibati ya kimataifa ya ubora wa daraja la juu itakayodumu kwa miaka mitatu.

Alisema kampuni ya kimataifa ya ACM ilifanya ukaguzi huo wa ubora wa huduma Agosti mwaka jana kwenye kanda nane na vituo vya mauzo, na matokeo ya ukaguzi huo yalithibitika kuwa huduma zinazotolewa zinafuata miongozo ya juu ya kimataifa na matakwa ya mamlaka ya udhibiti nchini.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afya punde zinapojiri.
NEEMA KWA WAKINAMAMA WAJAWAZITO NCHINI NEEMA KWA WAKINAMAMA WAJAWAZITO NCHINI Reviewed by By News Reporter on 3/09/2018 01:15:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.