Loading...

'SOMO KWA WAHITIMU WA VYUO VIKUU'

Loading...
Muhitimu mmoja wa aina yake wa elimu ya Chuo Kikuu katika Kitivo cha Mikrobiolojia kutoka katika Chuo Cha Federal Polytechnic Oko, aliamua kujiajiri mwenyewe kama fundi mwashi ili aweze kupata chakula cha kila siku, kipindi akiendelea kusubiri fursa ya ajira.

Lakini hii imekuwa tofauti kwa wahitimu wengi wa Chuo Kikuu ambao wanaamini ili iwe ajira hata ya kukidhi hitaji lake dogo lazima itoke kwenye fani aliyosomea tu na si vinginevyo.

Kwa Adimorah imekuwa tofauti yeye aliamua kufanya kazi ambayo kwa upande mwingine wahitimu wanaichukulia kama kujidhalilisha na kujishusha hadhi.

Akiandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagrama kama Ushauri kwa wahitimu wote waliokosa ajira alisema: "Mbali na kuwa muhitimu katika kitivo cha Microbiology. Ninaamini katika Kufanya KAZI ndio upate RIZIKI. Kama haitakuumiza, haiwezi kukulipa! Ninawapa changamoto wahitimu wote leo. KAMWE USIBWETEKE KUSUBIRI KAZI NZURI ZA OFISINI. KABLA HAZIJAJA, TOKA NJE KAANGAIKE. MUNGU ANABARIKI WATU WANAOANGAIKA MITAANI"

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika punde zinapojiri.
'SOMO KWA WAHITIMU WA VYUO VIKUU' 'SOMO KWA WAHITIMU WA VYUO VIKUU' Reviewed by By News Reporter on 3/01/2018 07:30:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.