Loading...
Hivi karibuni majuma kadhaa kupita msanii huyo alikuwa akiomba msaada wa pesa kupitia vyombo mbalimbali vya habari ili arudi hospitali ili akafanyiwe upasuaji wa goti lilikuwa likimsumbua sana na kufikia hatua ya kuandika na kusambaza mtandaoni waraka maalum kwa Rais Magufuli, akiomba msaada na Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth walichanga kiasi cha Milioni 15 na kumpatia msanii huyo kupitia katibu wake kwa ajili ya kwenda India kwa matibabu. Na hatimaye matibabu yamefanyika na anarudi salama kutoka nchini India.
Hata hivyo, mjumbe wa bodi Chama Cha Waigizaji Taifa (TDFAA TAIFA ), Lydia Mgaya anawasisitiza Leo saa saba mchana waigizaji kujitokeza kwa wingi kumpokea ndugu yetu mwigizaji mwenzetu 'Wastara Issa' ambaye anarudi Leo toka matibabu India.
Hata hivyo, mjumbe wa bodi Chama Cha Waigizaji Taifa (TDFAA TAIFA ), Lydia Mgaya anawasisitiza Leo saa saba mchana waigizaji kujitokeza kwa wingi kumpokea ndugu yetu mwigizaji mwenzetu 'Wastara Issa' ambaye anarudi Leo toka matibabu India.
Alisema: "Ni jambo la kumshukuru Mungu sana kwenda kutibiwa kwa msanii mwenzetu na kurudi salama tuonyeshe umoja wetu waigizaji wote kwakuwa Mungu mwema, pia nichukue fursa hii kuishukuru Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. John Pombe Magufuli ahsante sana kwa kugharamia matibabu na Wastara kurudi katika furaha na aweze kulitumikia taifa pia nawashukuru sana Watanzania mliojitoa wenye mioyo mema Mungu awabariki sana mlipotoa Mungu akawajaze maradufu."
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
'TUJITOKEZE KWA WINGI WASANII KUMPOKEA MWENZETU LEO SAA 7 MCHANA' - LYDIA MGAYA
Reviewed by By News Reporter
on
3/01/2018 09:00:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: