Loading...

VIGANJA 54 VYA BINADAMU VYAOKOTWA KATIKA BEGI

Loading...
Jozi ya viganja 27 vya binadamu vimekutwa katika kisiwa kimoja huko Siberia. Huku ikiwa ni kimoja tu kati ya viganja hivyo ndio kilikutwa ndani ya begi katika kisiwa hicho cha barafu karibu na mto Amur, nje kidogo na mji wa Khabarovsk.

Mwenyeji mmoja hapo mwanzo, alikuta kiganja kimoja nje kabla ya kukuta begi ambalo lilikuwa na viganja vilivyobakia katika eneo maarufu kwa uvuvi, ikiwa ni kilometa 30 karibu na boda ya China na Urusi, kwa mujibu wa Siberia Times

Wenyeji waliwaambia wachunguzi kuwa hivi karibuni hawajaona tukio lolote baya. Polisi kwa sasa wanajaribu kuchunguza nani wahusika wa vianja hivyo, lini vilikatwa na kwanini. Alama za vidole zimeonekana kwa kiganja kimoja tu mpaka sasa. Siberia Times iliripoti. Haikowazi kwamba huenda alama za vidole katika viganja vingine zilitolewa ili kupoteza ushahidi au la.

Wengine wanasema huenda viganja hivyo vilikatwa kutoka kwa wezi ikiwa kama adhabu na baadhi wanasema huenda viganja hivyo vimetoka hospitalini.

Kitendo hiko kimeshtua jamii kwamba huenda kuna biashara ya kusafirisha viungo vya binadamu inaendelea na huku mpaka sasa bado hawajatangaza taarifa rasmi ya kinachoendelea.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kimataifa punde zinapojiri.
VIGANJA 54 VYA BINADAMU VYAOKOTWA KATIKA BEGI VIGANJA 54 VYA BINADAMU VYAOKOTWA KATIKA BEGI Reviewed by By News Reporter on 3/11/2018 11:24:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.