Loading...

ZIMBABWE WAANDAA SHINDANO LA UREMBO KWA WATU WENYE UALBINO KWA MARA YA KWANZA

Loading...
Nchi ya Zimbabwe kwa mara ya kwanza imeandaa mashindano ya urembo ya watu wenye ualbino ili kuongeza elimu kuhusu watu wenye ulemavu wa ngozi.

Katika mashindano hayo kwa mara ya kwanza mrembo Sithembiso Mutukura, ameibuka mshindi wa mwaka 2018, kwa mara ya kwanza na kuandika historia.

Mutukura mwenye miaka 22, ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe aliwashinda washiriki wenzake 12. Mutukura alisema: "Lazima tuendelee kusimamia haki zetu na ushindi wangu utawanyanyua wasichana wadogo. Watu wenye ulemavu wasijishushe hadi wenyewe."

Na shindano hilo lilitarajiwa kuanza mwaka iliopita lakini kwa sababu ya ufinyu wa bajeti ndio uliperekea kukwamisha tukio hilo. Na inatarajiwa kuwa tukio la kila mwaka ili kuongeza elimu ya haki za watu wenye ualbino.

Watu wenye ualbino wanawindwa na kuuliwa kila mwaka katika sehemu tofauti za bara, hasa Tanzania na Zimbabwe.
Na Neema Joshua.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za burudani punde zinapojiri.
ZIMBABWE WAANDAA SHINDANO LA UREMBO KWA WATU WENYE UALBINO KWA MARA YA KWANZA ZIMBABWE WAANDAA SHINDANO LA UREMBO KWA WATU WENYE UALBINO KWA MARA YA KWANZA Reviewed by By News Reporter on 3/20/2018 11:17:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.