Loading...

APORWA GARI NA RAFIKI YAKE WA MTANDAONI

Loading...
Tapeli mmoja aliyetumia urafiki wa mitandao ya kijamii ili kutekeleza utapeli, ameshikiliwa na polisi baada ya kujaribu kuiba gari ya mtu ambaye alidaiwa kukutana naye katika mitandao ya kijamii. Polisi katika jiji la Tshwane wasimulia.

Polisi walisema muathirika alimualika tapeli huyo nyumbani kwake huko Queenwood, Mashariki ya Pretoria siku ya Ijumaa baada ya kufahamiana kupitia mtandao.

"Kufuatiwa na unywaji wa pombe, muathirika alimpatia ofa ya usafiri asubuhi na mapema Jumamosi. Katikati ya safari wakiwa safarini, mshukiwa huyo alimtishia kitu chenye nchi kali kabla ya kufanikisha uporaji huo wa gari aina ya Hyundai T20," Kapteni Daniel Mavimbela alisema katika kauli yake.

Mshukiwa wa uporaji alikamatwa akiwa hospitalini baada ya kufikishwa hospitalini hapo kwa kugonga gari moja hapo jirani na hospitali kupata majeraha kadhaa.

Muathirika wa uporaji alifikishwa hospitalini baada ya kuumizwa vibaya na kitu chenye ncha kali.

Mshukiwa wa uporaji atafikishwa mahakamani hivi mapema.

Polisi waliitaadharisha umma kuwa ni vyema kuwa makini na marafiki wa mitandaoni kwa kuwa wote sio wema ila wengine ni wahalifu.
Na Neema Joshua.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika punde zinapojiri.
APORWA GARI NA RAFIKI YAKE WA MTANDAONI APORWA GARI NA RAFIKI YAKE WA MTANDAONI Reviewed by By News Reporter on 4/09/2018 05:10:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.