Loading...
MSANII wa muziki wa dansi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Werrason yupo nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya shoo Jumamosi hii katika fukwe za Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Muda mfupi uliopita mwanamuziki huyo alipata fursa ya kuzungumza na waandishi wa habari katika kikao kilichofanyika katika fukwe hizo ambapo amesema hapa nchini anamfahamu Msanii Diamond Platnumz pekee maana amekuwa akimsikia mara kadhaa akitajwa huko Congo.
Hivyo amewaomba wasanii wa hapa nchini wamtafute kuanzia leo ili wabadilishane mawazo na hata ikiwezekana kufanya klabo ya pamoja kabla ya siku yake ya kufanya shoo yake hiyo ya Jumamosi na ile ya Jumanne katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
“Waafrika ni kitu kimoja hivyo ningependa wiki hii moja ambayo nipo hapa nipate kubadilishana mawazo na wasanii wa hapa Tanzania, ila hata kama kuna mtu angependa tufanye ngoma ya pamoja nipo tayari kwani kufanya hivyo ni kukuza muziki wetu wa Afrika ambapo utapata promo ya nchi nyingi jirani,” alisema Werrason.
Na Catherine Kisese.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za burudani punde zinapojiri.

WERRASON KULIAMSHA DUDE JUMAMOSI HII KATIKA FUKWE ZA ESCAPE ONE
Reviewed by By News Reporter
on
4/09/2018 05:26:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: