Loading...
Madaktari nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wamesema watarejelea mgomo wa nchi nzima siku ya Jumatatu ijayo Aprili 23 mwaka huu.
Jopo la madaktari limetoa tangazo Alhamisi wiki hii kuwa hatua zote zimefuatwa, na kwamba Waziri Mkuu wa nchi hiyo Bruno Tshibala amepewa barua yenye mapendekezo yaliyokubaliwa na pande zote mbili, lakini hakuna majibu yoyote ametoa.
Madaktari wanadai nyongeza ya mishahara yao pamoja na malipo ya ziada wanapofanya kazi katika mazingira magumu.
Licha ya kutanganzwa mgomo huo, madaktari wamesema kuanzia siku ya Jumatatu ambao watapewa matibabu ni wagonjwa wa dharura pekee na wale waliolazwa hospitalini.
Na Hamisi Fakhi.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika punde zinapojiri.

MADAKTARI KUENDELEA NA MGOMO DRC
Reviewed by By News Reporter
on
4/21/2018 08:19:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: