Loading...
Mark Zuckerberg mmiliki wa mtandao wa kijamii wa Facebook ameamua kufunguka na kumjibu mkurugenzi wa kampuni ya simu ya Apple, Tim Cook kwa lawama nzito alizomtupia kuhusu namna wanavyoshughulikia utunzaji wa taarifa za siri za wateja wao. Aliziita lawama za Cook ni 'Zinauzushi Sana'.
Mfarakano baina ya wakubwa hao ndani ya mji wa Silcon Valley ulianza wiki iliyopita wakati Cook alipoulizwa, Je! Angefanya nini kama yeye angepewa nafasi ya Zuckerberg huku kashfa ya Cambridge Analytica ikijitokeza. Alijibu na kusema "Nisingekuwa katika hali hii."
Mkurugenzi huyo wa Apple alienda mbali na kuishutumu mtandao huo wa kijamii kuwarushia matangazo wateja zake kwa kutumia data zao za siri. Pointi yake kubwa ilikuwa ni kwamba mitandao ya kijamii ni bure, lakini ili iendelee kubaki hivyo lazima wauze matangazo kwa watumiaji wa mtandao kwa kutumia taarifa zao binafsi na bila shaka, Zuckerberg atalitetea hili.
Katika onesho la Podcast linaloendeshwa na Ezra Klein ambalo urushwa na mtandao wa Vox, Zuckerberg alijibu kwa kusema sio vyote alivyosema mkurugenzi wa Apple ni kweli kwa maana kuendesha mtandao wa kijamii unabeba mabilioni ya watu ni gharama kubwa sana lakini sisi tunafanya kazi kwa nguvu zetu zote kuhakikisha tunawachaji wateja wa matangazo kiasi kidogo ila kwa wingi, Ila yapo makampuni yanayofanya kazi kwa nguvu kwachaji pesa nyingi wateja.
Kupitia kashfa ya Cambridge Analytica, Facebook imepoteza zaidi ya dola $40 milioni za kimarekani za wanahisa wake.
Na Peter Godwin.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za teknolojia punde zinapojiri.

MMILIKI WA FACEBOOK AMJIBU MKURUGENZI WA APPLE SKATA LA CAMBRIDGE ANALYTICA
Reviewed by By News Reporter
on
4/03/2018 10:14:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: