Loading...
Jaji wa jimbo la Philadelphia ambaye alimuhukumu rappa Meek Mill kwenda jela miaka 2 - 4, mwezi Novemba 2017, kwa kukiuka masharti katika kesi yake ya madawa ya kulevya na silaha ya mwaka 2009, amekataa kutoa rufaa ya kesi hiyo ili rappa huyo atoke jela kwa dhamana.
Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama zilizopatikana na mtandao wa New York Daily News, Jaji Genece Brinkley aliamua uamuzi huo baada ya kuogopa kuhusishwa katika kesi ya rappa huyo.
"Wapingaji walipata notisi ya mashtaka yote ya mtuhumiwa pamoja na kusikiliza kwa mapana zaidi," jaji Brinkley aliandika. "Hukumu iliyotolewa haikuzidi mipaka na mahakama ilitoa sababu madhubuti kwa nini hukumu hiyo ilitolewa ya miaka 2 mpaka 4."
Brinkley pia alikataa shutuma za yeye kuamua kesi hiyo kwa kupendelea upande wake binafsi katika kesi hiyo baada ya mwanasheria wa Meek Mill, Joe Tacopina kudai alimsukuma rappa huyo kuondoka katika kampuni iliyokuwa ikimsimamia. Alisema hakuna ushahidi hata kidogo wa madai hayo, na mahakama ilirudia mara kwa mara kuwa hatuweza kukupa huduma za kipekee kwa kuwa umechagua kuwa msanii.
Na Neema Joshua.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.

RUFAA YA RAPPA MEEK MILL YAKATALIWA
Reviewed by By News Reporter
on
4/03/2018 10:54:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: