Loading...
Mtu mmoja mwenye miaka 31, ameiambia mahakama kuwa aliambiwa na mganga wa kienyeji avute Bangi ili apone maradhi yaliyo msumbua kwa muda mrefu.
Felix Lisimba Mwerese alikamatwa Machi 27 saa tisa alhasiri katika jimbo la Ruaka akiwa na misokoto mitano ya Bangi.
Lisimba aliiambia mahakama kwamba alikuwa na matatizo ya tumbo kwa takribani miaka kumi, na mganga alimwambia akatumie bangi kama tiba.
"Nimekuwa naumwa mwili mzima, hasa tumboni, ninapo kula tu chakula na tumbo linaanza kuniuma. Nishazunguka katika hospitali nyingi sana na bila kupata suluhu ya tatizo langu. Ndipo nilipofanya uamuzi wa kwenda kwa mganga wa kienyeji na mganga alinishauri nitumie bangi," aliiambia mahakama wakati wa utetezi wake.
Mwerese aliachiliwa kwa dhamana ya Sh5,000 pesa za Kiganda, mpaka kesi yake itakapo sikilizwa tena Julai 12.
Na Hamis Fakhi.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika Mashariki punde zinapojiri.

MTU ALIYEAMBIWA NA MGANGA ATUMIE BANGI KAMA TIBA AFIKISHWA MAHAKAMANI
Reviewed by By News Reporter
on
4/09/2018 02:38:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: