Loading...

NI MUHIMU KUJIPONGEZA KWA KILA HATUA UNAYOIVUKA - Na Siri ya Utajiri

Loading...
Kwa wiki nzima ninaamini kuna kitu umefanya kuelekea kufanikisha MALENGO yako.  Kuna zoezi moja muhimu unapaswa kuwa unalifanya kila baada ya kuwa umefanikisha  kuchukua HATUA fulani. Tunatambua hatua moja ina MCHANGO mkubwa sana katika safari yako ya kufikia malengo yako.

Hivyo basi kutokana na umuhimu huo unapaswa kutenga muda wa kufikiri juu ya hatua ambazo umefanikisha kuzichua, kwa mfano kwa wiki nzima hii inayoisha leo angalia nini umefanya kama hatua muhimu ya kufanikisha malengo yako.  Baada ya tathimini hiyo JIPONGEZE  kwa hatua ulizozitekeleza.

Zoezi la kujipongeza ni MUHIMU kila unapofanikisha kutekeleza HATUA moja uliyokuwa umeipanga. Kwa kujipongeza unaongeza HAMASA ya kufanya zaidi na pia unatambua uwezo wako kwamba UNAWEZA na umefanikisha kutekeleza ulichokipanga.

Kujipongeza huku hatumaanishi uandae sherehe bali hata kujitamkia MANENO MAZURI ya kujipongeza  kwa kile ulichokifanya inatosha.

You Deserve The Best!
Vicent Stephen


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata makala za siri ya utajiri punde zinapojiri.
NI MUHIMU KUJIPONGEZA KWA KILA HATUA UNAYOIVUKA - Na Siri ya Utajiri NI MUHIMU KUJIPONGEZA KWA KILA HATUA UNAYOIVUKA - Na Siri ya Utajiri Reviewed by By News Reporter on 4/09/2018 03:04:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.