Loading...

SIONI WIVU DIAMOND KUMKUMBATIA HAMISA MOBETO - WEMA SEPETU

Mwanamitindo na mama wa wawili, Hamisa Mobetto na msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ’Diamond’ wamezua gumzo mitaani na mtandaoni katika tukio la utoaji tuzo za filamu za Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF) baada ya kukumbatia mbele ya alaiki ya watu, ambapo muigizaji Wema Sepetu alidai kuchukulia kawaida.

Diamond na Mobeto katika tuzo hizo zilizofanyika juzi katika ukumbi wa Mlimani City , walikwenda kama wageni waalikwa, walichaguliwa kukabidhi tuzo kwa mshindi wa kipengele cha ‘Best Original Music’ ambayo ilikwenda kwa filamu ya Safari ya Gwalu.

Katika kipengele hicho watu walikuwa wanasubiri kwa hamu kuona namna gani Wema ataweza kukabidhiwa tuzo na wawili hao, kwa kuwa filamu yake ya ‘Heaven Sent’ ilikuwa ni mojawapo iliyokuwa ikishindanishwa lakini bahati ndiyo hivyo haikuwa yake.

Akizungumzia namna alivyochukulia  kitendo cha Mobetto na Diamond kufika eneo hilo na kuweza kukabidhi tuzo, Wema ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Diamond miaka kadhaa iliyopita na hivi karibuni kuelezwa kwamba wamerudiana, amesema kitendo hicho kwake amekichukulia kawaida kwa kuwa Mobetto na Diamond ni mtu na mzazi mwenzake.
Loading...
tyle="font-size: 15px;">
"Wee ulitaka nichukuliaje labda, Mobetto na Diamond hawa ni wazazi jamani , ulitaka nikasirike au,halafu isitoshe mimi sina uhusiano wa kimapenzi na Diamond  bali ni washkaji tu na siyo kama watu wanavyosema," amesema Wema.

Kuhusu hatua yake ya kupata tuzo mbili ya msanii bora wa kike na chaguo la watu (People's Choice Award) kupitia filamu yake ya 'Heaven Sent', Wema amesema amefurahi kuona majaji wameweza kuona kipaji alichonacho.

Pia, aliahidi kuendelea kuwapa mashabiki wake kazi nzuri na kuwaondoa hofu wadau wa filamu waliokuwa wanasema kuwa bongo movie imekufa kuwa siyo kweli bali ilikuwa imelala tu.


Hata hivyo, hakusita kutoa shukurani kwa mashabiki zake ambao amesema ni  kati ya watu ambao waliweza kushiriki kumpigia picha hadi kuhakikisha anapata ushindi huo.
Na Geofrey Okechi.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
SIONI WIVU DIAMOND KUMKUMBATIA HAMISA MOBETO - WEMA SEPETU SIONI WIVU DIAMOND KUMKUMBATIA HAMISA MOBETO - WEMA SEPETU Reviewed by By News Reporter on 4/03/2018 08:27:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.